Psalms 124

Shukrani Kwa Ukombozi Wa Israeli

Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi.

1 aKama Bwana asingalikuwa upande wetu;
Israeli na aseme sasa:
2kama Bwana asingalikuwa upande wetu,
wakati watu walipotushambulia,
3 bwakati hasira yao ilipowaka dhidi yetu,
wangalitumeza tungali hai,
4 cmafuriko yangalitugharikisha,
maji mengi yangalitufunika,
5maji yaendayo kasi
yangalituchukua.

6 Bwana asifiwe,
yeye ambaye hakuruhusu turaruliwe kwa meno yao.
7 dTumeponyoka kama ndege
kutoka mtego wa mwindaji;
mtego umevunjika,
nasi tukaokoka.
8 eMsaada wetu ni katika jina la Bwana,
Muumba wa mbingu na dunia.
Copyright information for SwhNEN